...Kwa hakika enzi za kati zilishuduwa na masimulizi ya hadithi nyingi, hatahivyo kuna hadithi zilianza kutoweka kama ile hadithi ya Nyoka mbawa yenye asili ya mji wa Franche Komte. Hadithi yetu inaanzia katika maeneo ya kandokando ya mto Luwe. Ni mto unaopatikana katika eneo la Jura na maeneo ya Mutie UT Piekh.
Awali ya yote, hebu tuanze kusimulia habari za kiumbe huyu, inasemekana kwamba ni nyoka mkubwa mwenye mabawa makubwa yanayofanana na popo, mwendo wake ni wa kasi zaidi ya umesa akijitafautisha kwa kuwa na jicho moja tu katikati ya kichwa chake. Kiukweli hilo sio jicho halisi, hilo ni jiwe kubwa jekundu linalofahamika kwa jina la Yakuti iliyong aa. Jiwe hili ni kivutio cha kila mwenye tamaa. Kiukweli nyoka huyu ana nguvu za ajabu sana. Kulingana na baadhi ya masimulizi, mtu yoyote anaefanikiwa kulinyakua jiwe hilo hupata utajiri wa milele...