Tazama, anapita: mwenye ngozi ya kahawia, nywele nyingi mwilini, uso wenye ndevu na miguu yenye nywele, akiwa amevaa kofia yake kubwa na akiwa uchi kabisa…
Anazurura akitafuta asali na tumbaku… msichana aliyepotea msituni au labda msafiri fulani ambaye atamdanganya kwa mluzi wake au kwa kuiga mlio wa kifaranga… Huyo ndiye Pombero, Pombero yule wa hadithi anayezurura usiku huko Misiones. […] Matendo yake ni ya kutisha. Hata hivyo, wakati mwingine humpenda msafiri fulani na anaweza hata kumwokoa hatarini. Lakini pia anajua jinsi ya kuwafanya wasafiri wapotee njia au hata wafe kwa hofu mbele yake. […]
[…] Hutembea kwenye njia nyekundu za Misiones, akitafuta mawindo yake miongoni mwa walowezi na wakataji miti. Mara nyingi uthubutu wake huwa mkubwa sana hivi kwamba hufanikiwa hata kumtongoza msichana mdogo kutoka mitaa ya pembezoni mwa mji wowote.
Huyo ndiye Pombero, mmoja wa wahusika wa hadithi za mapokeo za Misiones.
Wengi wamemsikia; lakini ni wachache tu—wachache sana—waliowahi kumwona. Lakini ukweli ni huu: kwa karibu miaka mia tatu sasa, Misiones imekuwa makao yake.