Huyo anapita: mwenye ngozi nyeusi, mwili wenye manyoya mengi, ndevu, na miguu yenye manyoya; amevaa kofia yake kubwa, na yuko uchi kabisa... Anaenda kutafuta asali na tumbaku... huenda akamtafuta mwanamke kijana aliyepotea msituni, au labda msafiri atakayemvutia na kumpoteza njia kwa miluzi yake au sauti ya kifaranga... Huyo ni Pombero; yule Pombero wa ngano ambaye huzunguka-zunguka usiku katika eneo la Misiones. [...] Matendo yake ni ya kutisha. Hata hivyo, wakati mwingine humpenda msafiri fulani na anaweza hata kumwokoa kutoka hatarini. Lakini pia ana uwezo wa kuwapoteza watu njia au kuwafanya wafe kwa hofu kutokana na uwepo wake. [...] [...] huzunguka-zunguka katika njia zenye udongo mwekundu wa Misiones, akiwatafuta mawindo yake miongoni mwa walowezi na wakata-miti; mara nyingi ujasiri wake hufikia hatua ya kumfanya afanikiwe kumshawishi hata msichana mdogo kutoka pembezoni mwa mji wowote. Huyo ndiye Pombero, mmoja wa wahusika wa ngano za jadi za Misiones. Wengi wamehisi uwepo wake; wachache wachache sana wamemwona. Hata hivyo, ukweli unabaki kuwa amekuwepo Misiones kwa karibu miaka mia tatu.  | Entry #39044 — Variant: Not specifiednone
|
Tazama, anapita: mwenye ngozi ya kahawia, nywele nyingi mwilini, uso wenye ndevu na miguu yenye nywele, akiwa amevaa kofia yake kubwa na akiwa uchi kabisa… Anazurura akitafuta asali na tumbaku… msichana aliyepotea msituni au labda msafiri fulani ambaye atamdanganya kwa mluzi wake au kwa kuiga mlio wa kifaranga… Huyo ndiye Pombero, Pombero yule wa hadithi anayezurura usiku huko Misiones. […] Matendo yake ni ya kutisha. Hata hivyo, wakati mwingine humpenda msafiri fulani na anaweza hata kumwokoa hatarini. Lakini pia anajua jinsi ya kuwafanya wasafiri wapotee njia au hata wafe kwa hofu mbele yake. […] […] Hutembea kwenye njia nyekundu za Misiones, akitafuta mawindo yake miongoni mwa walowezi na wakataji miti. Mara nyingi uthubutu wake huwa mkubwa sana hivi kwamba hufanikiwa hata kumtongoza msichana mdogo kutoka mitaa ya pembezoni mwa mji wowote. Huyo ndiye Pombero, mmoja wa wahusika wa hadithi za mapokeo za Misiones. Wengi wamemsikia; lakini ni wachache tu—wachache sana—waliowahi kumwona. Lakini ukweli ni huu: kwa karibu miaka mia tatu sasa, Misiones imekuwa makao yake.  | Entry #39517 — Variant: Not specifiednone
|
Huko anakwenda: mweusi, mwenye manyoya mengi, uso wenye ndevu, miguu yenye manyoya mengi, akiwa amevaa kofia yake kubwa na akiwa uchi kabisa... Anatafuta asali na tumbaku... labda msichana aliyepotea msituni au labda msafiri yeyote ambaye atamdanganya kwa mluzi wake au kwa mlio wa kifaranga cha kuku... Ni Pombero; Pombero wa kizushi anayezurura katika usiku za Misiones. [...] Matendo yake ni ya kutisha. Ingawa wakati mwingine hupendezwa na msafiri na anaweza hata kumuokoa kutoka hatarini. Lakini pia anajua jinsi ya kuwapoteza au kuwafanya wafe kwa hofu mbele ya uwepo wake.[...] [...] anatembea kwenye njia nyekundu za Misiones, akitafuta mawindo yake kati ya wakoloni na wakata miti, na mara nyingi ujasiri wake huwa mkubwa kiasi kwamba hata anafanikiwa kumshawishi msichana fulani kutoka vitongoji vya pembezoni mwa jiji lolote. Hivyo ndivyo alivyo Pombero, mmoja wa hadithi maarufu za Misiones. Wengi wamemsikia, wachache, wachache sana, wamemuona. Lakini ukweli ni kwamba kwa karibu miaka 300 sasa anaishi Misiones.  | Entry #39578 — Variant: Not specifiednone
|